Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Oktoba 7, 2019


Makampuni ya kamari yameongeza dau juu ya uwezekano wa kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kufutwa kazi baada ya kukubali kichapo cha kushtukiza dhidi ya Newcastle. Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anapigiwa upatu kuchukua mikoba ya Solskjaer.

Winga wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs anaamini Ole Gunnar Solskjaer anatakiwa kusajili wachezaji wengine watano ili timu irejee kwenye kiwango chake.

Winga wa Chelsea Christian Pulisic,21, anaripotiwa kutaka kuomba kutolewa kwa mkopo kama hatapata muda mwingi zaidi wa kucheza klabuni hapo.

Kocha wa Arsenal Unai Emery anapiga hesabu za kumnunua beki wa Wolves Willy Boly. Wolves wanaweza kutaka dau la pauni milioni 20, wao walimnunua nyota huyo raia wa Ivory Coast kwa pauni milioni 10. (Sun)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amedokeza kuwa mrithi wake klabuni hapo atakuwa kocha wa Rangers ya Uskochi Steven Gerrard ama kocha wa zamani wa klabu hiyo forme Kenny Dalglish.

Steven Gerrard na Kenyy Dalgish wote wameichezea Liverpool kwa mafanikio makubwa. (Star)

Beki wa zamani wa Liverpool Glen Johnson amemshauri mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 26, tkuihama klabu yake na kumpigia chapuo ajiunge na Man City. (Manchester Evening News)

Real Madrid wapo tayari kuchuana na Juventus ikatika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili kiungo mkabaji wa Chelsea N'Golo Kante. Vigogo hao wa La Liga wanaweza kulipa dau la uasajili la kufikia pauni milioni 70 ili kumnasa Mfaransa huyo. (Sport)

AC Milan walikuwa kwenye mipango ya kutaka kumfuta kazi kocha Marco Giampaolo wakati wa mapumziko wa mechi dhidi ya Genoa siku ya Jumamosi. Mpaka mapumziko Genoa walikuwa wakiongoza kwa goli moja lakini mchezo uliisha kwa Milan kupata ushindi wa 2-1 (SempreMilan)

Beki wa zamani wa pembeni wa Manchester United Alexander Buttner, 30, amesema alikataa maombi ya usajili kutoka klabu za Uskochi za Celtic na Rangers kabla ya kuamua kutimkia Marekani katika klabu ya New England Revolution. (Goal)

Callum Wilson, Bournemouth

Kocha wa klabu ya Bournemouth Eddie Howe amemtaka mshambuliaji wake Callum Wilson kuzipa kisogo tetesi kuwa Man United inataka kumsajili mwezi Januari. (
Daily Echo)

Mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa Gabriel Agbonlahor, ambaye ndiye mshika rekodi ya kupachika mabao mengi zaidi kwa Villa amefichua kuwa wapinzani wao wa jadi klabu ya Birmingham City walijaribu kumsajili kutoka klabu ya Villa Park wakati alipokuwa mdogo. (Birmingham Live)

Nyota wa zamani wa klabu ya Liverpool Steve McMahon amemdokeza kocha Jurgen Klopp kumsajili kiungo wa Leicester City James Maddison kabla ya wapinzani wao. (Stadium Astro).

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Oktoba 7, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Oktoba 7, 2019 Reviewed by Zero Degree on 10/07/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.