Loading...

Adhabu ya kuvujisha picha au video zisizo na maadili



Kufuatia kuvuja kwa video zisizo na maadili mitandaoni zikimuonyesha mwanafunzi anayedaiwa kusoma chuo cha usimamizi wa fedha, Wakili Getrude Diabene amesema kisheria ni kosa kujirekodi picha au video za utupu kabla hata kusambazwa.

Wakili Getrude Diabene amesema ikitokea picha au video kusambaa mitandaoni huwa wanaangalia imetokea kwenye mazingira gani, kisha wanaenda kwenye kanuni ambazo zinasema mtu huyo alikuwa na nia gani ya kusambaza, kama alikuwa ana nia ya kumdhalilisha mwenziye inakuwa kosa kisheria.

"Ukija kwenye sheria ya makosa ya mitandaoni kifungu cha 14 kinasema ni kosa kusambaza video au picha zenye kuashiria ngono, tena wote wawili mnakuwa mmefanya kosa, adhabu yake ni miaka zaidi ya 10 jela, faini ya milioni 30 au vyote kwa pamoja, aliyesambaza atakuwa na kosa la jinai" amesema Wakili Getrude Diabene

Aidha Wakili huyo ameongeza kusema kwenye tukio kama hilo huwa kuna mambo mawili ambayo yanatokea kwa sababu kuna wale wanaotaka kurekodi wenyewe, pili kuna kurekodiwa bila ya kujua au kutekwa na kuleweshwa halafu unarekodiwa.
Adhabu ya kuvujisha picha au video zisizo na maadili Adhabu ya kuvujisha picha au video zisizo na maadili Reviewed by Zero Degree on 9/24/2020 07:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.