Loading...

Mitandao kote duniani yakumbwa na matatizo

Hali ilivyokuwa katika uwanja wa ndege wa Milwaukee, Wisconsin, wakati tatizo la mitandao lilipotokea Julai 19, 2024

Mashirika ya ndege, benki, vituo vya televisheni na biashara nyingine duniani kote zilikuwa zikijitahidi kukabiliana na mojawapo ya matatizo makubwa zaidi ya kimtandao katika miaka ya hivi karibuni leo Ijumaa, ambayo yanaonekana kusababishwa na jaribio la kuimarisha programu ya kuzuia virusi.

Mashirika makubwa ya ndege ya Marekani hapo awali yalisitisha safari zote za ndege kutokana na changamoto za mawasiliano -- ingawa kampuni ya American Airlines baadaye ilisema kuwa imerejesha safari zake.

Viwanja vya ndege kote ulimwenguni vilisema mifumo ya kompyuta ilikuwa ikikumbwa na matatizo, na kupelekea ucheleweshwaji wa huduma za safari za ndege.

Kampuni ya Microsoft ilisema kwenye tovuti yake kwamba matatizo yalianza siku ya Alhamisi, yakiathiri watumiaji wa huduma ya Azure inayoendesha programu ya usalama wa mtandao ya CrowdStrike Falcon.
Mitandao kote duniani yakumbwa na matatizo Mitandao kote duniani yakumbwa na matatizo Reviewed by Zero Degree on 7/20/2024 05:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.