Loading...

INASEMEKENA KUWA HAWA NDO WAPINZANI WA FACEBOOK, CHEKI HAPO CHINI


Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.

Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz amesema kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga kuhudumia marafiki 90 tu.
Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia vifurushi.
Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya mitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.
Paul Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya Vermont amesema kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzani.
Hata hivyo kuhusiana na baadhi ya watu kuuiita kwa jina bandia la anti-Facebook mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao wenye mtazamo wake binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.
INASEMEKENA KUWA HAWA NDO WAPINZANI WA FACEBOOK, CHEKI HAPO CHINI INASEMEKENA KUWA HAWA NDO WAPINZANI WA FACEBOOK, CHEKI HAPO CHINI Reviewed by Zero Degree on 10/01/2014 11:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.