Loading...

CHELSEA YAMTAKA MESSI KWA PAUNI MILIONI 200


Picha: Mmiliki wa club ya chelsea Roman Abromovich

Lionel Messi ameambiwa kwamba kuna mkataba wa miaka sita kutoka kwa kilabu ya Chelsea unaomngojea.
Duru za karibu na mchezaji huyo wa Barcelona zinaarifu kuwa Chelsea imeweka wazi kwamba iko tayari kutoa kitita cha pauni millioni 200 kumnunua nyota huyo.
Vilevile The Blues imedaiwa kwamba iko tayari kulipa mahitaji yake ya mshahara ambayo huenda yakaongeza kiwango hicho mara mbili.
Picha: Nyota wa club ya Barcelona Lionel Messi

Mnamo mwezi Novemba kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikana habari zinazoihusisha kilabu hiyo na Messi,lakini katika kilabu ya Barcelona kumekuwa na mgogoro tangu wakati huo na ripoti kutoka Uhispania zinasema kuwa mchezaji huyo amekuwa akizozana na muajiri wake Luis Enrique.
Inadiwa kuwa Mesi hakushiriki katika mazoezi ya siku ya jumatatu huku Enrique akishindwa kukana mgogoro uliopo kati yake na Messi.

Credits: BBC
CHELSEA YAMTAKA MESSI KWA PAUNI MILIONI 200 CHELSEA YAMTAKA MESSI KWA PAUNI MILIONI 200 Reviewed by Zero Degree on 1/08/2015 07:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.