Loading...

Aliyetongoza kupitia Facebook afungwa jela


Labrie Owen alikuwa akishindana na wenzake nani atashiriki ngono zaidi

Mwanaume mmoja 20,aliyetumia Facebook kumtongoza mwanafunzi mwenza kwa nia ya kushiriki ngono naye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela nchini Marekani.





Owen Labrie alipatikana na hatia ya kumtongoza msichana huyo ambaye jina lake limebanwa kwa sababu ya umri wake mdogo wa miaka 15.
Labrie na msichana huyo walikuwa wanafunzi wa shule moja ya kifahari sana mjini Concord, New Hampshire.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo, wakili wa mshtakiwa alidai kuwa ni desturi ya wanafunzi wanaokamilisha masomo kuwaalika wanafunzi wapya shuleni humo kisha wakashiriki ngono nao katika tamaduni inayojulikana kwa jina la uzushi ''kupiga saluti''
Shule hiyo ya kifahari na ghali ya St Paul inajivunia kuwa kitovu cha elmu kwa mamia ya viongozi wa kada mbalimbali nchini Marekani akiwemo waziri wa maswala ya kigeni John Kerry.
Wanafunzi wengine waliosomea katika shule hiyo ya ''Kupiga saluti'' ni mabalozi 13 na watafiti wenye hadhi ya juu duniani.
Image captionLabrie Owen sasa sharti asajiliwe kama mtu aliyewahi kuwadhulumu watoto kijinsia
Wakili wa msischana huyo aliiambia mahakama kuwa Labrie alijigamba kwa maswahiba wake kuwa alikuwa 'amepigia saluti' msichana huyo na hivyo kumsababishia fedheha miongoni mwa wanafunzi wake.
Katika kujitetea wakili wa Labrie aliomba mahakama imhurumie mteja wake kwani huo ulikuwa ujinga wa matineja waliokuwa mbioni wakitaka kukubalika na wenzao.
Jaji wa mahakama ya juu Larry Smukler alimtaja Labrie kuwa 'muongo wa kupindukia' alipotoa hukumu hiyo ya mwaka mmoja gerezani.

Credits: BBC

Aliyetongoza kupitia Facebook afungwa jela Aliyetongoza kupitia Facebook afungwa jela Reviewed by Zero Degree on 10/30/2015 11:08:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.