Loading...

Paul Ryan ateuliwa spika wa bunge Marekani


Mwanasiasa wa chama cha Republican nchini Marekani Paul Ryan ameteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani.

Ryan, anayetoka jimbo la Wisconsin, hakutaka sana kuwania mwanzoni lakini mwishowe alijitosa kwenye kinyang’anyiro na akaungwa mkono na wengi wa wabunge wa Republican katika Bunge la Congress kumrithi John Boehner aliyetoka Ohio.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 45 alikuwa mgombea mwenza wa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican Mitt Romney mwaka 2012.
Amesaidia kuamua sera ya bajeti na uchumi katika bunge la Congress na amesema alitaka kuchukua wadhifa huo ili kuunganisha wanachama wa chama cha Republican.

Romney RyanImage copyrightAP
Image captionMitt Romney (kushoto) akiwa na Paul Ryan

Kwenye wadhifa huo wake mpya, yeye ndiye wa pili sasa katika safu ya wanaoweza kumrithi rais nyuma ya makamu wa rais.
Miongoni mwa majukumu mengine, spika wa bunge nchini Marekani husimamia shughuli za bunge la chini la Congress katika masuala ya kiutawala na kibiashara.
Paul Ryan ateuliwa spika wa bunge Marekani Paul Ryan ateuliwa spika wa bunge Marekani Reviewed by Zero Degree on 10/30/2015 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.