Chelsea na Arsenal zabanduliwa League Cup
Masaibu ya Jose Mourinho msimu huu yaliendelea baada ya vijana wake kubanduliwa kutoka shindano la League Cup na Stoke City kupitia mikwaju ya penalti mechi iliyochezwa Jumanne usiku.
Arsenal pia hawakuwa na bahati kwani walitupwa nje baada ya kuchapwa 3-0 na Sheffield Wednesday.
Arsenal, waliofanya mabadiliko saba kwenye timu iliyolaza Everton 2-1 Jumamosi, walipata matatizo zaidi kwani Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain waliondoka uwanjani baada ya kuumia dakika 20 za kwanza. Mechi yote walikuwa na makombora mawili pekee yaliyolenga goli.
Uwanja wa Brittania, baada ya Chelsea kudhibiti mpira kipindi cha kwanza ambacho hakikuzaa bao lolote, Stoke walitwaa uongozi kupitia Jon Walters dakika ya 52.
Loic Remy aliwaokoa Chelsea, japo kwa muda alipofunga bao dakika ya 90, sekunde chache kabla ya mchezaji wa Stoke Phil Bardsley kufukuzwa uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.
Stoke walifunga mikwaju yao yote, lakini Eden Hazard akakosa mkwaju wake uliokuwa wa mwisho, ambao ulizimwa na kipa Jack Butland.
Mashabiki waStoke walifurahia sana masaibu ya Mourinho na kumcheka, wengine wakisema huenda akafutwa Jumatano asubuhi.
Chelsea walilazwa 2-1 na West Ham Jumamosi katika mechi ambayo Mourinho alifukuzwa eneo wanamokaa makocha baada yake kumtafuta na kumzungumzia refa Jon Moss wakati wa mapumziko.
Credits: BBC
Chelsea na Arsenal zabanduliwa League Cup
Reviewed by Zero Degree
on
10/28/2015 12:05:00 PM
Rating: