Moja kwa moja: Magufuli akabidhiwa cheti Tanzania(Habari za hivi punde)
Msafara wa Bw Magufuli umelindwa vikali na maafisa wa usalama
11:30am: Msafara wa Rais mteule John Magufuli pamoja na ule wa Rais Jakaya Kikwete waelekea ikulu chini ya ulinzi mkali.
11:00am: Mgombea urais wa chama cha ACT Wazalendo Anna Mghwira aliyemaliza wa tatu ni miongoni mwa waliofika kumpongeza Bw Magufuli.
11:00am: Rais anayeondoka Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria hafla hiyo, sawa na kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan. Bw Jonathan amampongeza rais mteule.
11:10am: John Pombe Joseph Magufuli akabidhiwa rasmi cheti cha ushindi uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili Oktoba 25.
11:00am: Hafla ya kumkabidhi Magufuli cheti inafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Ukumbi huo umejaa watu hadi pomoni.
10:20am: Jeshi la Tanzania limeonekana likisafirisha magari ya kijeshi, wanajeshi na silaha hadi visiwani Zanzibar. Matokeo ya uchaguzi visiwani humo yalifutiliwa mbali na mwenyekiti wa tume Jecha Salim Jecha.
9.00am: Mgombea urais wa chama cha CCM John Magufuli leo anakabidhiwa cheti cha ushindi na tume ya uchaguzi baada yake kutangazwa mshindi Alhamisi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema kuwa Magufuli, alijipatia kura 8,882,935 ikiwa ni aslimia 58.46.
Mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema alijipatia kura 6,072,848 ikiwa ni asilimia 39.97 ya kura zote halali.
Baada ya kutangazwa kwa ushindi wake, wafuasi wake walisherehekea katika miji mbalimbali nchini humo.
Moja kwa moja: Magufuli akabidhiwa cheti Tanzania(Habari za hivi punde)
Reviewed by Zero Degree
on
10/30/2015 01:13:00 PM
Rating: