Mwanamke achaguliwa kuiongoza nchi ya Nepal
Bunge nchini Nepal limemchagua mtetezi wa haki za wanawake Bidhya Devi Bhandari kuwa rais wa kwanza mwanamke, katika hatua ambayo imetajwa kuwa ya kihistoria.
Yeye ndiye mtu wa pili kushikilia wadhifa huo ambao hata hivyo huwa hauna mamlaka makubwa.
Mwanamke huyo wa miaka 54 kwa sasa ndiye naibu mwenyekiti wa chama tawala cha kikomunisti cha Communist Party of Nepal (United Marxist Leninist).
Bi Bhandari alikuwa waziri wa ulinzi wa 2009 na 2011. Kama rais, ameahidi kutetea haki za makundi ya watu wachache pamoja na haki za wanawake nchini Nepa.
Mapema mwezi huu, bunge la Nepal lilimchagua waziri mkuu mpya
KP Sharma Oli.
Bi Bhandari atachukua nafasi ya Ram Baran Yadav, aliyekuwa rais wa kwanza wa taifa hilo kuchaguliwa na watu mwaka 2008 baada ya Nepal kufutilia mbali utawala wa kifalme.
Kuchaguliwa kwake kumejiri muda mfupi baada ya Nepal kuanza kutekeleza katiba mpya mwezi Septemba ambayo inatarajiwa kurejesha uthabiti katika taifa hilo la bara Asia.
Hata hivyo katiba hiyo imesababisha vurugu zilizopelekea kuuawa kwa watu karibu 40.
Katiba hiyo inaeleza taifa hilo lenye Wahindi wengi kuwa jamhuri isiyoongozwa na dini na ambayo imegawanywa katika majimbo saba.
Lakini makabila yanayoishi kusini mwa Nepal yanataka mamlaka majimbo hayo yapewe mamlaka zaidi.
Source: BBC
Mwanamke achaguliwa kuiongoza nchi ya Nepal
Reviewed by Zero Degree
on
10/29/2015 11:28:00 AM
Rating: