Ouattara ashinda uchaguzi Ivory Coast
Alassane Ouattara ameshinda uchaguzi wa urais nchini Ivory Coast kwa wingi wa kura. Matokeo yalitangazwa kupitia runinga huku rais huyo akishinda kwa asilimia 83.66.
Hii inamaanisha kwamba hakutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi.
Raia wa Ivory Coast waliamkia habari za ushindi wa Rais Alassane Outtara kama walivyotarajiwa kwamba rais huyo ataongoza kwa muhula mwengine wa miaka mitano.
Baada ya mwongo mmoja wa kutoimarika kwa uchumi na vita vya wenyewe kwa wenyewe, wengi watafurahia kwamba uchaguzi huo ulifanyika kwa amani.
Uchaguzi wa mwisho wa urais uliofanyika mwaka 2010 ulisababisha vita vya miezi mitano ambapo zaidi ya watu elfu 3000 waliuawa.
Rais wa zamani Laurent Gbagbo, yuko mjini the Hague katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita akingojea kesi inayomkabili.
Ijapokuwa rais huyo amekosolewa kwa kushindwa kuleta maridhiano na haki, amesifiwa kwa kuimarisha uchumi wa taifa hilo na kulifanya kuwa taifa lenye uchumi ulioimarika kama ilivyokuwa miaka ya sabini.
Credits: BBC
Ouattara ashinda uchaguzi Ivory Coast
Reviewed by Zero Degree
on
10/28/2015 11:56:00 AM
Rating: