UCHAGUZI 2015: YANAYOJRI TANZANIA
MATUKIO MBALI MBALI YA UCHAGUZI NCHINI TANZANIA YAKIWEMO MATOKEO YA UCHAGUZI
12.40pm:Chama cha Upinzani kisiwani Zanzibar CUF kimetoa taarifa kikisema kinasikitishwa na mda unaochukuliwa na tume ya uchaguzi kisiwani humo kutoa matokeo.Kimesema kuwa hakioni sababu ya tume hiyo kutoa matokeo nusu nusu licha ya kuwa matokeo ya majimbo yote 54 yamehesabiwa kujumlishwa na kutolewa.
12.19pm:Tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar imesitisha utangazaji wa matokeo kwa muda baada ya umeme kukatika. Hata hivyo imeahidi kuendelea na matokeo hayo baada ya umeme kurudi muda mfupi baadaye.
10.36am: Biashara zimeanza kufunguliwa mjini Dar es Salaam nchini Tanzania huku wengi wa wawafanyibiashara wakiendelea kufunga biashara zao. Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara wanasema kuwa wataendelea kuzifunga hadi rais mpya atakapotangazwa.
11.03am: Wanahabari wa vyombo vya ndani na nje ya nchi, pamoja na mawakala wa vyama vya siasa, wakiwa ndani ya ukumbi ambao Tume ya Uchaguzi Zanzibar inatangaza matokeo ya uchaguzi.
10.00am: Mawaziri watano waangushwa
Mawaziri watano wa serikali inayomaliza muda wake wameanguka kwenye uchaguzi katika majimbo yao,huku wagombea wengine wa Ubunge maarufu nao wakiangushwa na Kamba ya upinzani katika matokeo ya kura yanayoendelea kutolewa kufuatia uchaguzi mkuu nchini humo uliofanyika Jumapili.
Mawaziri hao watano wa serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete inayomaliza muda wake ni Stephen Wassira Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Dk Steven Kebwe Naibu Waziri wa Afya, Christopher Chiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayehusika na Uwekezaji na Uwezeshaji, Anne Kilango Malecela Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi na Omar Nundu aliyewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi.
Mawaziri hao walioangushwa katika majimbo yao wanaungana na wabunge wengine maarufu katika Bunge la Kumi la Tanzania waliong’ara ambao kwa sasa wameshindwa kurejea.
Hata hivyo pia wamo mawaziri wa Zamani Cyril Chami na Omary Nundu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania inaendelea kutangaza matokeo ya Ubunge na Urais.
9.00am: Matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Gando nchini Tanzania.
8.00am: Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Tanzania yanaendelea kutolewa huku BBC ikiendelea kukufahamisha kuhusu matukio tofauti nchini humo.
Tayari tume ya uchaguzi imetoa matokeo ya majimbo 24 na bado inaendelea kutoa mengine zaidi. Huko Zanzibar, visiwa ambavyo kando na kutawaliwa na Rais wa Jamhuri, huwa pia na rais wake, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufikia sasa imetangaza matokeo ya majimbo 13 kati ya majimbo 54 yaliyoko visiwani humo.
Unaweza kupata habari zaidi kuhusu uchaguzi huo wa Tanzania uliofanyika Jumapili kwa kubonyeza hapa Tanzania: #uchaguzi2015.
SIKU NJEMA
Credits: BBC
UCHAGUZI 2015: YANAYOJRI TANZANIA
Reviewed by Zero Degree
on
10/27/2015 01:19:00 PM
Rating: