Loading...

Uchaguzi TZ:Matukio mbali mbali yanavyojiri

MATUKIO MBALIMBALI YA UCHAGUZI NCHINI TANZANIA
10.00am:Kufikia sasa mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CCM John Pombe Magufuli anaendelea kuongoza katika kura zilizohesabiwa

Image captionTume ya uchaguzi nchini Tanzania

9.58pm:Rais mpya wa Tanzania kujulikana leo
Tume ya uchaguzi nchini Tanzania hii leo inatarajiwa kumtangaza rais mpya wa taifa hilo hii leo.Hatua hii inajiri siku moja tu baada ya Upinzani kupinga matokeo ya ucgaguzi huo kwa madai kwamba kulikuwa na udanganyifu mkubwa.Tayari tume ya uchaguzi Kisiwani Zanzibar imefutilia matokeo ya uchaguzi kisiwani humo.

Image captionMagazeti nchini Tanzania

9.33am: Yalio maagazetini nchini Tanzania.
9.30am:Marekani imelaani hatua ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais pamoja na wajumbe wa bunge la wawakilishi visiwani humo.

Image captionMakamishna

9.15am:Makamishna wa tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar wameushtumu uamuzi wa mwenyekiti wao Jecha Salum Jecha kwa kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa kiswa hicho bila ya kuwashauri
9.00am:Tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar inajiandaa kutangaza tarehe mpya ya marudio ya uchaguzi huo.

Image captionKisiwani Zanzibar

6.15am:Kisiwani Zanzibar
HABARI YA ASUBUHI
Uchaguzi TZ:Matukio mbali mbali yanavyojiri Uchaguzi TZ:Matukio mbali mbali yanavyojiri Reviewed by Zero Degree on 10/29/2015 11:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.