Loading...

Uganda imeondoa jeshi lake Sudan Kusini


Vikosi vya Uganda viliingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mwaka wa 2013 kufuatia mwaliko wa rais Salva Kiir

Kundi la mwisho la wanajeshi wa Uganda waliosalia nchini Sudan Kusini wameondoka nchini leo.

Hii ni kulingana na taarifa ilotolewa na wakuu wa jeshi.
Mojawepo wa kipengee kwenye mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya serikali na waasi mwezi agosti,kiliwataka wanajeshi wote waondoke Sudan Kusini.
Vikosi vya Uganda viliingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mwaka wa 2013 kufuatia mwaliko wa rais Salva Kiir
Image copyrightBBC World Service
Image captionTakriban wanajeshi 4,000 wa UPDF walikuwa mjini Bor Kaskazini mwa mji mkuu wa Juba.
Kikosi cha mwisho kinatarajiwa kuondoka Sudan Kusini leo.
Hadi sasa haijabainika Uganda ilikuwa na wanajeshi wangapi nchini humo ila kinachofahamika ni kuwa takriban wanajeshi 4,000 wa UPDF walikuwa mjini Bor Kaskazini mwa mji mkuu wa Juba.
Mchango wao katika makabiliano hayo yanategemea upande upi unaelezea kwani kuna wale wanaoilaumu kwa kuunga mkono Salva Kiir dhidi ya makamu wake wa zamani Riek Machar.
Wengine wanasema kuwa kuwepo kwao kulipunguza hatari ya mauaji ya kimbari haswa ikizingatiwa kuwa vita hivyo vilichukua mkondo wa kikabila.
Hata hivyo mchakato ulioleta amani uliwataka waondoke na sasa wakati umewadia.
Swali ibuka ni je hali itakuwaje baada ya wanajeshi hao kuondoka ?
Image copyrightReuters
Image captionMchakato ulioleta amani uliwataka waondoke na sasa wakati umewadia.
Je nani atachukua lawama iwapo vita na mauaji yatatokea ?
Jeshi hilo la Uganda lilikuwa linastahili kurithiwa na kikosi cha majeshi ya muungano wa Afrika.
Kikosi hicho bado hakijaundwa.
Uganda hata hivyo itakuwa na kikosi kidogo nchini humo kama sehemu ya muungano unaokabiliana na wanamgambo wa Lords Resistance Army.

Source: BBC
Uganda imeondoa jeshi lake Sudan Kusini Uganda imeondoa jeshi lake Sudan Kusini Reviewed by Zero Degree on 10/30/2015 11:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.