UN kutaja mataifa yanayochafua mazingira
Inadaiwa kuwa joto limeongezeka kwa zaidi ya kipimo cha nyuzi joto mbili, na kuhatarisha zaidi sayari ya dunia.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya inayotarajiwa kutangazwa na Umoja wa Mataifa.
Umoja huo unatarajia kuchapisha mpango mpya wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Mpango huo umewasilishwa na mataifa 146, yanapojiandaa kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa.
Ripoti hiyo inatazamiwa kuelezea kwa mapana na marefu zaidi hali ya sasa ya mazingira katika mataifa ambayo hayataweza kuzuia kuongezeka kwa kiwango cha joto kwa sasa duniani.
Umoja huo vilevile unatarajiwa kuelezea waziwazi mataifa kadhaa tajiri au maskini ambayo yamesaidia kupunguza hewa chafu ya Carbon Dioxide.
UN kutaja mataifa yanayochafua mazingira
Reviewed by Zero Degree
on
10/31/2015 07:39:00 AM
Rating: