UN yawafuta kazi watu 5 kwa utovu wa nidhamu
Wafanyikazi wanne wa umoja wa mataifa wamefutwa kazi baada ya kupatikana na hatia ya kutizama na kusambaza filamu ya ngono kupitia mtandao wa intanet wa shirika hilo la kimataifa.
Kibarua cha mfanyikazi mwengine kiliota nyasi baada ya kupatikana na kosa la kusafirisha kilo 173 ya bangi katika gari la kazi.
Visa hivyo vyote vilifanyika kati ya Julai mosi mwaka uliopita na juni tarehe 30 mwaka huu.
Hata hivyo ripoti hiyo ya UN haijabainisha iwapo walifunguliwa mashtaka au la.
Ripoti hiyo hutolewa na shirika hilo kwa lengo la kutoa tathmini ya wafanyikazi wake 41,000 na kuonesha hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi yao.
Hata hivyo taarifa hiyo haisemi walikokuwa wanafanya kazi na tarehe kamili waliofutwa kazi.
Msemaji wa UN, Farhan Haq, aliiambia BBC kuwa kesi zote dhidi ya wafanyikazi wa umoja wa mataifa hushughulikiwa na afisi moja tu.
Mfanyikazi mwengine alifutwa kazi baada ya kuiba dola 2,200 kutoka kwenye mkoba wa abiria.
Alikuwa analinda uwanja wa ndege uliokuwa unasimamiwa na shirika hilo.
Mwengine alibeba abiria kwenye gari la UN bila idhini huku mwengine akifukuzwa kazi baada ya kuwaruhusu waandishi wa habari kuingia katika eneo wasiloruhusiwa.
Source: BBC
UN yawafuta kazi watu 5 kwa utovu wa nidhamu
Reviewed by Zero Degree
on
10/31/2015 07:40:00 AM
Rating: