Loading...

Je Pistorius ataongezewa kifungo leo?

Oscar Pistous

Mahakama kuu ya rufaa nchini Afrika Kusini huenda ikaamua leo hii iwapo Mwanariasha mlemavu wa miguu Oscar Pistorius amehusika na mauaji ama aliuua bila kukusudia wakati alipomfyatulia risasi mpenziwe wakati sikukuu ya wapendanao ulimwenguni mnamo mwaka 2013.

Mwanariadha huyo mwenye ulemavu wa miguu , hivi karibuni ameanza kutumikia kifungo cha nyumbani akiwa tayari amekwisha kutumikia kifungo cha mwaka mmoja kati ya miaka mitano aliyohukumiwa kutumikia.
Endapo majaji wa mahakama hiyo kuu ya rufaa watageuza maamuzi ya awali na kuwa kesi ya mauaji ,mkimbiaji huyo maarufu atarejeshwa tena jela na kutumikia kifungo cha miaka kumi na mitano .

Image copyrightBBC World Service
Image captionMarehemu Reeva Steenkamp

Ni takribani siku arobaini tangu mwanariadha huyo alipooachiwa kutoka jela kutumikia kifungo cha nyumbani. Oscar Pistorius ana uwezekano kukabiliwa na kifungo cha muda mrefu. Kama upande wa mshataka ambayo ni Jamuhuri itashinda kwenye rufaa kosa la mwanariadha huyo litabadilika na kutoka kosa la kuua bila kukusudia na kuwa kosa la mauaji.
Hata hivyo mfukuza upepo huyo mwenye umri wa miaka 28 hatakuwepo mahakamani. Anafuatilia kesi yake kutoka katika nyumba ya kifahari ya mjomba wake iliyopo Pretoria ambapo anamalizia kifungo cha miaka mnne kilichobaki.
Hajajulikana nini kitakachotokea katika kesi hiyo inayosikilizwa na majaji watano lakini ifahamike masuala ya kisheria ni ya kiufundi zaidi.
Hoja za Upande wa Mashataka ambayo ni Jamuhuri ni kwamba Jaji aliyesikiliza kesi hiyo Thokozile Masipa hakuwa sahihi kuona kuwa mwanariadha huyo alitenda kosa la mauaji ya kutokusudia kwa madai kwamba mwanaridha alijua madhara ya tendo alilolifanya.
Pestorius anatuhumiwa kufyatua risasi mara nne kwenye bafu iliyokuwa imefungwa ambapo anatuhuhumiwa kuwa alijua tendo hilo lingeweza kusababisha kifo.
Hata hivyo mwanariadha huyo amekuwa akijitetea kuwa alidhani kuwa alivamiwa na wezi na kwamba alidhani mpenzi wake Reeva Steenkamp alikuwa yupo chumbani.
Upande wa mashataka unapinga kuwa hoja na kusema mwanariadha huyo alikusudia kuua.

Source: BBC
Je Pistorius ataongezewa kifungo leo? Je Pistorius ataongezewa kifungo leo? Reviewed by Zero Degree on 11/03/2015 10:33:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.