Loading...

Magufuli amteua Majaliwa kuwa waziri mkuu mpya!

Mbunge wa Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu mpya.
Rais wa Tanzania John Magufuli amemteua mbunge wa Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu mpya.

Tangazo la uteuzi wa Bw Majaliwa limetolewa bungeni na Spika Job Ndugai. Bunge limeahirishwa kwa dakika 45 kuwapa muda wabunge kuchambua uteuzi huo kabla ya kurejea na kupiga kura.
Bw Majaliwa amekuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa, Jimbo la Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) tangu 2010.
Eneo la Ruangwa linapatikana kusini mashariki mwa Tanzania. Alikuwa naibu waziri katika ofisi ya Waziri Mkuu aliyehusika na utawala wa mikoa na serikali za mitaa katika serikali ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Alihudumu pia kama naibu waziri wa elimu.



Share this news all your beloved friends!!!!!!!!
Magufuli amteua Majaliwa kuwa waziri mkuu mpya! Magufuli amteua Majaliwa kuwa waziri mkuu mpya! Reviewed by Zero Degree on 11/19/2015 11:44:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.