Loading...

Mkurugenzi Bunge afariki dunia


Dar es Salaam. Mkurugenzi Msaidizi wa Shughuli za Bunge, Hellen Mbeba (36) amefariki dunia ghafla wakati akiwahishwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ilisema Mbeba alifariki jana.
Akizungumza kwa njia ya simu, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema ofisi yake imepoteza mtendaji makini aliyekuwa akiandaliwa kuja kusimamia sheria za Bunge kwa nafasi ya juu zaidi.

Alisema msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Kisasa mjini Dodoma na taarifa zitaendelea kutolewa na ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu.







Mshirikishe na mwenzako!!!
Mkurugenzi Bunge afariki dunia Mkurugenzi Bunge afariki dunia Reviewed by Zero Degree on 11/28/2015 06:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.