Rais wa Zanzibar aongezewa muda
Rais wa Zanzibar, Ali Mohammed Shein
Muda wa kuhudumu wa rais wa kisiwa cha Zanzibar umeongezwa baada ya matokeo ya uchaguzi wa eneo hilo kufutiliwa mbali na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kufuatia madai ya udanganyifu.
Muda wa kuhudumu wa rais wa kisiwa cha Zanzibar umeongezwa baada ya matokeo ya uchaguzi wa eneo hilo kufutiliwa mbali na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kufuatia madai ya udanganyifu.
Muda wa Ali Mohammed Shein kuwa mamlakani ulitarajiwa kukamilika siku ya jumatatu.
Alikuwa akitafuta kuchaguliwa kwa awamu nyengine kama mgombea wa chama cha CCM,huku mpinzani wake wa karibu Seif Sharif Hamad akijitangaza mshindi wa shughuli hiyo iliofanyika tarehe 25 mwezi Octoba.
Rais anayeondoka madarakani amesema kuwa ataingilia kati ili kutafuta suluhu ya amani.
Wikendi iliopita ,mabomu mawili yalilipuka katika kisiwa cha Zanzibar,licha ya kuwa hakuna majeraha yalioripotiwa .
Mgombea urais wa upinzani kisiwani Zanzibar, Maalim Seif Hamad
Uchaguzi uliopita kisiwani humo,ambamo ni kikuvutio kikuu cha Utalii umekumbwa na ghasia.
Waandishi wanasema kuwa kuna wanajeshi wengi katika eneo hilo.
Bwana Hamad,mgombea wa upinzani kupitia chama cha UKAWA amewataka wafuasi wake kuwa watulivu na kufanya amani siku ya jumatatu huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Source: BBC
Rais wa Zanzibar aongezewa muda
Reviewed by Zero Degree
on
11/03/2015 10:48:00 AM
Rating: