Loading...

Watu 9 wauawa kinyama Burundi

Watu 7 wauawa kinyama Burundi
Watu wenye silaha wamewapiga risasi na kuwauwa watu 9 usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu wa Burundi- Bujumbura

Watu hao waliokuwa katika kilabu cha burudani mjini Bujumbura waliamrishwa walale chini kabla ya kufyatuliwa risasi na kuuawa papo hapo.
Meya wa mji huo ametaja kisa hicho kama mauwaji ya kinyama.
Waliwauawa 7 na kuwajeruhi wengine wawili alisema Freddy Mbonimpa meya wa mji huo.

Awali wenyeji wa vitongoji vya mji wa Bujumbura walionekana wakitoroka makwao kwa hofu

Mauaji hayo yanatukia katika siku ya mwisho iliyotolewa na serikali kwa raia walioko na silaha kuzisalimisha kwa vyombo vya dola.
Awali Serikali ilikuwa imewapa watu fursa ya kusalimisha silaha walizo nazo lau sivyo polisi wachukue hatua kali dhidi yao kuwapokonya.
Hapo jana wenyeji wa vitongoji vya mji wa Bujumbura walionekana wakitoroka makwao kwa hofu ya makabiliano na vyombo vya serikali.
Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura, aliwaona watu wamebeba magodoro na kadhalika katika mabarabara, wakihamia kwenda kwa marafiki na jamaa katika mitaa salama.
Katika juma lilopita pekee , watu 20 wamekufa, hasa kwenye mitaa ambako upinzani una nguvu.
Watu zaidi ya laki mbili wamekimbilia nchi za nje.
Katika juma lilopita pekee , watu 13 wamekufa, hasa kwenye mitaa ambako upinzani una nguvu.
Idadi ya watu waliouawa sasa imegonga 22 na kuongeza idadi ya awali ya watu 200 ambao wameuwawa katika wimbi la machafuko ya kisiasa nchini humo, tangu mwezi Aprili, pale rais Pierre Nkurunziza alipotangaza nia ya kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu.


Comment & Share this story:
Watu 9 wauawa kinyama Burundi Watu 9 wauawa kinyama Burundi Reviewed by Zero Degree on 11/08/2015 08:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.