Loading...

BALAA LA MWISHO WA MWAKA: Kasi ya ULANGUZI wa TIKETI katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo yatisha!!!


Dar es Salaam. Baadhi ya mawakala wa kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo (UBT) jijini Dar es Salaam, wanatuhumiwa kununua tiketi za mabasi kisha kuziuza kwa walanguzi ambao nao huwauzia wasafiri waendao mikoa ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa kwa Sh70,000.

Imedaiwa kuwa mawakala hao hujaza majina ya uongo kwenye vitabu sahihi vya tiketi ili kuonyesha kuwa mabasi yamejaa kitu ambacho siyo kweli.

Mwananchi jana ilifika kituoni hapo na kukuta wakala wa mabasi yendayo Kahama, Shinyanga, Mwanza, Arusha na Kilimanjoro akiwa amesimama na wasafiri waliokuwa wakitaka kwenda Mwanza.

Wakala huyo alimkaribisha mwandishi akijua ni msafiri, huku akitaka kufahamu anasafiri kwenda wapi na kumwambia kama ni Mwanza tiketi zimeisha.

“Unaelekea Mwanza, Moshi, Kahama au wapi?... Mwanza tiketi zimeisha kama unataka chukua namba yangu ya simu (alitaja) ikifika mchana nipigie nitakuwa nimekutafutia ... lakini utatakiwa kulipa Sh 70,000,” alisema.

Wakala huyo alisema kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Krisimas na Mwaka Mpya usafiri ni wa shida na ndiyo chanzo cha kupanda kwa nauli.

“Kama una shida ya kusafiri, ‘jiongeze’ (alipe zaidi ya nauli ya kawaida). “

Utasumbuka dada, kwanini nikufiche?... ukweli ni kwamba, magari hayajajaa, mawakala wanauza tiketi kwa walanguzi ambao wanaziuza kwa bei ya juu, kama kweli unataka kusafiri fanya hivyo, mimi hadi saa 7:00 mchana nitakuwa nimeipata uje kuchukua,” alisisitiza wakala huyo.

Hata hivyo, baada ya kuona mwandishi hawezi kununua tiketi kwa bei hiyo, alimtaka ataoe Sh50,000 ili apande basi la kawaida ambalo nauli yake ni Sh35,000.

Nauli halali ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza ni kati ya Sh35,000 hadi Sh45,000.

“Nimekuja kukata tiketi asubuhi nasafiri kesho kwenda Mwanza, lakini nimeambiwa tiketi halali zimeisha ila zipo za Sh80,000,” alilalamika Prisca Juma.

Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray alisema watahakikisha wanadhibiti ulanguzi huo wa tiketi unaodaiwa kufanyika katika kituo hicho cha mabasi Ubungo.


Credits: Mwananchi



Mshirikishe namwenzako kuhusu habari hii!!
BALAA LA MWISHO WA MWAKA: Kasi ya ULANGUZI wa TIKETI katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo yatisha!!! BALAA LA MWISHO WA MWAKA: Kasi ya ULANGUZI wa TIKETI katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo yatisha!!! Reviewed by Zero Degree on 12/21/2015 02:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.