Loading...

Dar es salaam: Chuo cha Aga Khan kujenga hospitali Kampala!!!


Chuo Kikuu cha Aga Khan kipo mbioni kukamilisha ujenzi wa hospitali itakayotoa huduma za kisasa sambamba na kufanya tafiti mbalimbali juu ya magonjwa na tiba nchini Uganda.


Hospitali hiyo itajengwa katika Makutano ya Barabara ya Jinja na New Port Bell katikati ya jiji hilo, hivyo kufikika kirahisi na wagonjwa pamoja na watumishi.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, uongozi wa chuo hicho umesema hospitali hiyo itakayokuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 600, itatanguliwa na hospitali ndogo itakayomudu kulaza watu 150 ifikapo mwaka 2020.

“Tukiwa na viwango vya kimataifa vya huduma za afya, tunatarajia kuwahudumia Waganda kama tunavyofanya kwingineko duniani katika kutibu magonjwa sugu na yale yanayohitaji umakini wa ziada. Tutakuwa na vifaa bora ili kuhakikisha afya za wananchi zinakuwa za uhakika,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inabainisha kuwa kukamilika kwa hospitali hiyo kutapunguza idadi ya wananchi wanaolazimika kusafiri nje ya nchi kufuata matibabu kutokana na miundombinu ya ndani kutokidhi mahitaji kwa kuwa vifaa vyote muhimu vitakuwapo.

Hospitali ya aina hiyo itakuwa ni ya pili kwa ukanda wa Afrika Mashariki baada ya ile iliyopo Nairobi. Kwa mujibu wa uongozi wa chuo, tayari hospitali zake za Karachi, Pakistan na Nairobi zimetunukiwa tuzo za ubora wa kimataifa kwa huduma za kisasa.

“...Chuoni hapo tutawaandaa madaktari, manesi, wakunga na watawala wa taasisi za afya ili kuboresha huduma kwa wananchi wanaowahudumia,” ilisema taarifa hiyo. Tuna imani, kwa kuweka mazingira mazuri ya tiba, madaktari wengi wazawa waliokimbilia nje ya nchi, watarejea nyumbani na kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kuwabakiza wahitimu wapya ambao wangeweza kukimbilia nje pia.”

Chuo hicho kimeahidi kutoa huduma kwa wote bila kujali tofauti ya kipato kwa kuandaa ufadhili maalumu kwa watu maskini ambao hawawezi kumudu gharama zake.



Credits: Mwananchi



Mshirikishe na mwenzako kuhusu habri hii!!
Dar es salaam: Chuo cha Aga Khan kujenga hospitali Kampala!!! Dar es salaam: Chuo cha Aga Khan kujenga hospitali Kampala!!! Reviewed by Zero Degree on 12/17/2015 08:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.