Loading...

Mbeya: Wachina wakutwa na nyara za serikali zenye thamani ya zaidi 900milioni, watupwa jela miaka 20!!!

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mbeya imewahukumu raia wanne wa China kwenda jela miaka 20 kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na nyara za serikali za thamani ya zaidi Sh900milioni.


Kuhusu faini kwa kosa hilo, Hakimu Mkazi Michael Mteite amesema Wachina hao wanatakiwa kulipa mara kumi ya thamani ya pembe za faru walizokutwa nazo ambacho ni kiasi cha sh9bilioni.

Hata hivyo, wakili wa washtakiwa hao, Ladislaus Rweikaza amesema kuwa ataisoma nakala ya hukumu hiyo na kisha kujadiliana na wateja wake ili kujua iwapo watakata rufaa ama la. Hata hivyo, mwanasheria huyo amesema kuwa hukumu kwa wateja wake haimaanishi kuwa imetolewa kwa misingi ya ubaguzi bali inatokana na kosa walilokutwa nao raia hao.




Credits: Mwananchi




Mshirikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!
Mbeya: Wachina wakutwa na nyara za serikali zenye thamani ya zaidi 900milioni, watupwa jela miaka 20!!! Mbeya: Wachina wakutwa na nyara za serikali zenye thamani ya zaidi 900milioni, watupwa jela miaka 20!!! Reviewed by Zero Degree on 12/17/2015 08:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.