Loading...

Dar es salaam: Mwanafunzi UDSM auawa baada ya kupigwa risasi!!!

Tukio hilo lilitokea jana usiku majira ya saa mbili baada ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia duka moja lililopo maeneo aliyokuwepo yeye na kupora simu, vocha na fedha taslimu.



mwanafunzi
Mwanafunzi wa UDSM, Mutaengerwa Mafwiri enzi za uhai wake.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mutaengerwa Mafwiri ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi jana usiku eneo la Msewe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na www.globalpublishers.co.tz kwa njia ya simu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camillus Wambura amekiri kutokea kwa tukio hilo.


Kwa mujibu wa Kamanda Wambura tukio hilo lilitokea jana usiku majira ya saa mbili baada ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia duka moja lililopo maeneo hayo na kupora simu, vocha na fedha taslimu kiasi cha shilingi 100,000/=.

Wakati wakiondoka eneo la tukio wananchi walianza kuwapigia kelele ndipo walipoanza kupiga risasi ovyo ambapo mojawapo ilimpata Mafwiri aliyekuwa katika banda la chipsi na kumsababishia umauti.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na uchunguzi bado unaendelea.



Credits: Global publishers




Mshirikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!

Dar es salaam: Mwanafunzi UDSM auawa baada ya kupigwa risasi!!! Dar es salaam: Mwanafunzi UDSM auawa baada ya kupigwa risasi!!! Reviewed by Zero Degree on 12/16/2015 10:43:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.