Loading...

Mkuu wa mkoa wa KILIMANJARO ala X-MASS gerezani!!!



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala     


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala amesherehekea Krismasi kwa kula chakula na wafungwa na mahabusi katika Gereza la Karanga, Moshi.

Wafungwa na mahabusi 1,900 walichinjiwa ng’ombe na kupikiwa wali pamoja na kupatiwa vinywaji baridi.

Kabla ya kula chakula hicho jana, Makala alishuhudia fainali ya mechi ya soka kati ya timu ya mahabusi na wafungwa.

Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dk Juma Malewa alisema ana miaka zaidi ya 20 ndani ya magereza lakini hakuwahi kushuhudia tukio alilolifanya Makala.

Makala aliwataka wafungwa wanapomaliza kutumikia vifungo vyao warejee uraiani wakiwa raia wema na kuwa mabalozi wazuri wa kupambana na uhalifu.

Mkuu wa Gereza la Karanga, Hassan Mkwiche alisema kutokana na upendo alionao, amechagua wafungwa na mahabusi kuwa familia yake katika kusherehekea sikukuu.

Mkwiche alisema kwa ufadhili wa mfanyabiashara, Patrick Ngiloi, Makala aliwaletea kilo 60 za mchele, ng’ombe, masanduku 38 ya soda na lita 40 za mafuta ya kupikia.


Katika sherehe hiyo, Makala aliikabidhi kombe timu ya mahabusi (Barcelona FC) baada kutwaa ubingwa kwa kuifunga wafungwa (Umoja FC) bao 1-0.


Credits: Mwananchi


Mshirikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!
Mkuu wa mkoa wa KILIMANJARO ala X-MASS gerezani!!! Mkuu wa mkoa wa KILIMANJARO ala X-MASS gerezani!!! Reviewed by Zero Degree on 12/26/2015 08:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.