Loading...

Paul Makonda ashikiriwa na TUCTA kwa udhalilishaji ni baada ya kuwaweka ndani kwa saa sita maofisa ardhi kwa kisingizio cha kaulimbiu ya Rais John Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’.



Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
Dar es Salaam. Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limelaani watendaji wa Serikali katika ngazi mbalimbali kuwakandamiza na kuwadhalilisha wafanyakazi kwa kisingizio cha kaulimbiu ya Rais John Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’.


Akitoa tamko hilo Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Hezron Kaaya alisema hivi karibuni vimeibuka vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya wafanyakazi hususan wa serikalini, jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za kazi.

Alisema watendaji hao wakiwamo wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na viongozi wengine wamekuwa wakitoa vitisho na kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji wafanyakazi walio chini yao kwa madai ya kutekeleza agizo la kufanya kazi.

Akitolea mfano tukio la hivi karibuni la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuwaweka ndani kwa saa sita maofisa ardhi waliochelewa kufika katika eneo la kazi kama ilivyotakiwa.

Alisema kitendo cha kuwaweka ndani wafanyakazi hao ni kinyume na haki za binadamu kwani walistahili kuwajibishwa kwa utovu wa nidhamu si kuswekwa mahabusu.

“Kosa walilofanya ilikuwa ni utovu wa nidhamu kazini, hivyo walipaswa kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kazi siyo kuwadhalilisha namna ile, ndiyo maana tunamtaka Makonda kuomba radhi.

Kaaya aligusia pia na suala la wafanyakazi wa mkoa wa Kilimanjaro kuzuiwa kwenda likizo na kudai kuwa agizo hilo ni kinyume na taratibu za kazi.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla kusitisha likizo na ruhusa zote kwa watumishi wake katika kipindi cha siku kuu za Krismasi na Mwaka mpya na kuwataka waendelee kuchapa kazI.

“Hakuna mtu anayeweza kuzuia mfanyakazi asiende likizo kama mwajiri unahisi unataka mfanyakazi wako aendelee kuwapo kazini taratibu zipo, mnajadiliana na mnakubaliana lakini si kulazimisha.

Tumeshtushwa sana na kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ndiyo maana tunasema kuna viongozi wanataka kupotosha dhana ya Magufuli wakati mwenyewe ameitoa kwa nia njema kabisa”a lisema Kaaya.

Juzi Makalla alifafanua suala hilo na kueleza kuwa hajasitisha likizo kwa wafanyakazi wote wa umma bali ni wakuu wa wilaya, wakurugenzi na watendaji wa idara mbalimbali ambao wanatakiwa kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli mpaka Januari mwakani.

Alipotakiwa kujibu hoja hiyo, Makonda alisema hana muda wa kujadili matamko na yuko tayari kuchukua hatua yoyote kuhakikisha haki inatendeka kwa wananchi.

“Wanatoa tamko sidhani kama walichukua hatua kujua kilichotokea na watu wangapi wamepoteza maisha kutokana na migogoro ya ardhi, wanatetea haki za binadamu bila kuangalia ni binadamu wangapi wamekandamizwa haki zao,” alisema.
Nikiwa mkuu wa wilaya nasema nitachukua hatua yoyote kutatua kero za wananchi kuhakikisha wanapata haki inayostahili,” alisema Makonda.

Kuhusu tamko la msajili wa hazina, Lawrence Mafuru la kuyataka mashirika ya umma yanayojiendesha kwa hasara kupunguza wafanyakazi, Kaaya alisema nayo ni mojawapo ya kauli za kuwanyanyasa wafanyakazi.


Credits: Mwananchi




Mshirikishe na mwenzako kuhusiana na habari hii!!!!
Paul Makonda ashikiriwa na TUCTA kwa udhalilishaji ni baada ya kuwaweka ndani kwa saa sita maofisa ardhi kwa kisingizio cha kaulimbiu ya Rais John Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’. Paul Makonda ashikiriwa na TUCTA kwa udhalilishaji ni baada ya kuwaweka ndani kwa saa sita maofisa ardhi kwa kisingizio cha kaulimbiu ya Rais John Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’. Reviewed by Zero Degree on 12/03/2015 09:53:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.