Loading...

Sherehe za sikukuu za X-Mass zapigwa marufuku nchini SOMALIA!!!


Serikali ya Somalia imepiga marufuku sherehe za kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi katika mji mkuu wa Mogadishu.




Wapiganaji wa Kundi la Al Shabaab.

Mkurugenzi mkuu katika wizara ya masuala ya dini, Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya kuwa maadhimisho kama hayo yasiyofungamana na dini ya Kiislamu yanaweza kusababisha mashambulizi kutoka kundi la wanamgambo wa Al Shabab.

“Maofisa wote wa kulinda usalama wanapaswa kusimamisha ama kuvunja mikutano ya aina yoyote yenye nia ya kuadhimisha sikukuu hiyo isiyofungamana na dini ya Kiislamu.” alisema Sheikh Mohamed

Mwaka uliopita wapiganaji wa Al shabab walishambulia kambi ya majeshi ya muungano wa Afrika (AU) iliyopo Mogadishu wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Krismasi.

Wanajeshi 5 waliuawa katika shambulizi hilo la kuvizia.

Asilimia kubwa ya raia wa Somalia ni wasilamu.


Credits: Global publishers
ZeroDegree.
Sherehe za sikukuu za X-Mass zapigwa marufuku nchini SOMALIA!!! Sherehe za sikukuu za X-Mass zapigwa marufuku nchini SOMALIA!!! Reviewed by Zero Degree on 12/23/2015 06:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.