Loading...

Hii ndio TASWIRA ya jiji la Dar na shamra shamra za maandalizi ya sikukuu!!!



Taswira ya baadhi ya mitaa ya katikati ya Kariakoo, Dar ilivyofurika umati wa watu.


Harakati za hapa na pale zikiendelea katika mitaa ya Msimbazi, Kariakoo.


Baadhi ya wakazi wa Dar wakichangamkia kununua nguo za sikukuu kwenye mitaa ya Kongo na Msimbazi.


Barabara ya Msimbazi ambayo imejengwa na kampuni ya ujenzi ya Strabag ilivyoonekana kufurika watu kwa kuuzia bidhaa chini.


Harakati zikiendelea katika barabara ya Msimbazi, Kariakoo.


Hali halisi ya maeneo ya mitaa ya Kariakoo ilivyokuwa kila mahali.



ZIKIWA zimebaki siku mbili waumini wa dini ya Kikristo duniani kusherehekea sikukuu ya Krismas ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, leo kwa wingi wao, wameonekana wakifanya manunuzi ya nguo na bidhaa mbalimbali za sikukuu katika mitaa ya Kariakoo.

Kamera yetu imefanikiwa kunasa baadhi ya picha zinazoonesha wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wakiwa katika shamrashamra za manunuzi na kusababisha mitaa kutokupitika kwa urahisi kutokana na msongamano wa watu.



ZeroDegree.
Hii ndio TASWIRA ya jiji la Dar na shamra shamra za maandalizi ya sikukuu!!! Hii ndio TASWIRA ya jiji la Dar na shamra shamra za maandalizi ya sikukuu!!! Reviewed by Zero Degree on 12/23/2015 06:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.