KIA yaokoa MABILONI ya fedha ndani ya kipindi cha wiki moja kwa kukamata NYARA za Serikali zilizokua zikitoroshwa!!!
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kadco, Bakari Murusuri alisema juzi kuwa Desemba 15, mwaka huu walimkamata raia mwenye asili ya Asia kwenye Uwanja wa Kia akiwa na madini ya Tanzanite kilo 2.04 yenye thamani isiyopungua Sh2 bilioni akiyasafirisha kwenda nje.
Murusuri alisema raia huyo alikuwa akitaka kutorosha madini hayo kinyume cha utaratibu wa nchi na saa chache baadaye walimkamata raia mwingine wa kigeni akiwa na kucha za simba 261 na meno 60 ya wanyama hao.
“Abiria hawa walikuwa wakisafiri kwa ndege ya Qatar na walipofika uwanjani tuliwatilia shaka, na tulipowakagua waligundulika wakiwa na nyara za Serikali,” alisema Murusuri.
Alisema Desemba 18, mwaka huu walimkamata raia mwingine wa kigeni akitaka kutorosha pembe mbili za twiga na Desemba 19 waliwakamata watu wawili wakiwa na pembe mbili za swala.
Kaimu mkurugenzi huyo alisema watuhumiwa hao walifikishwa kituo cha polisi kilichopo uwanjani hapo na kwamba, taratibu nyingine za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao.
“Wote tulifanikiwa kuwakamata katika upekuzi wa kawaida wa ndani ya uwanja wetu, maofisa wetu wa usalama wanafanya kazi nzuri ili kuhakikisha wanakamata abiria wanaotaka kutorosha nyara za Serikali,” alisema Murusuri.
Meneja huyo alisisitiza kuwa mifumo ya udhibiti wa utoroshaji nyara za Serikali iko imara.
Credits: Mwananchi
Mshirikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!
KIA yaokoa MABILONI ya fedha ndani ya kipindi cha wiki moja kwa kukamata NYARA za Serikali zilizokua zikitoroshwa!!!
Reviewed by Zero Degree
on
12/23/2015 07:10:00 PM
Rating: