Loading...

Sheria za ardhi ndio kikwazo kwa wakulima.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Morogoro. Wakulima wadogo wilayani Kilosa wameonekana kukosa ufahamu wa sheria za ardhi, jambo linalowafanya kushindwa kufuatilia kwa makini masuala ya ardhi pale inapotokea migogoro katika maeneo yao.

Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Miradi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Adam Nyaruhuma alisema hayo katika mkutano wa wakulima wadogo wilayani humo, juu ya utafiti kuhusu migogoro ya ardhi alioufanya na kugundua upungufu uliopo.

Dk Nyaruhuma alisema katika utafiti wake aligundua upungufu uliojitokeza ukiwamo utoaji elimu kwa wakulima kutoka kwa wataalamu mbalimbali.

Alitaja upungufu mwingine kuwa ni wananchi kutokuwa na uelewa juu ya Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 pamoja na Sera ya Ardhi ya mwaka 1995 ambayo iliboreshwa mwaka 1997.

Mtafiti huyo aliiomba Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji juu ya masuala ya ardhi ambayo yamekuwa yakisababisha kuwapo kwa migogoro ya mara kwa mara wilayani Kilosa.

Pia, alisema kutokana na uelewa huo wa wananchi, hasa vijijini ifike wakati kila mwananchi mwenye kipande cha ardhi kipewe hati ya umiliki ili kupunguza au kuondoa kabisa migogoro inayojitokeza.

“Kutokana na kuwapo kwa migogoro baadhi ya upungufu wa sheria unaruhusu vijiji kimoja hadi vitatu kukaa pamoja na kumiliki ardhi kwa mkataba wa pamoja. Ni vyema Serikali ikaendelea kufanya marekebisho ya mara kwa mara,” alisema.

Dk Nyaruhuma alisema sheria hairuhusu kufanya shughuli za kilimo au ufugaji katika vijiji bila kuwa na cheti cha kimila cha umiliki wa ardhi.

Wakizungumza katika mkutano huo, wakulima Andrew Kikule na Sara Kalunde walisema endapo Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji, migogoro katika maeneo yao itamalizika. “Tumekuwa na migogoro katika wilaya yetu kutokana na kutokuwa na mpangilio wa kueleweka na kila upande unajiona kuwa na haki ya kumiliki,” alisema Kikule.


Credits: Mwananchi


Comment & Share this story!!
Sheria za ardhi ndio kikwazo kwa wakulima. Sheria za ardhi ndio kikwazo kwa wakulima. Reviewed by Zero Degree on 12/29/2015 03:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.