Ubungo hali ni shwari sasa, swala la ULANGUZI WA TIKETI limekwisha!!!
Gazeti hili lilifika kituoni hapo jana na kukuta utulivu wa hali ya juu ikilinganishwa na siku tano zilizopita.
Pia ofisi za mabasi hazikuwa na foleni kama ilivyokuwa mwanzoni na wasafiri walikuwa wakikata tiketi kama kawaida.
Baadhi ya mawakala na makarani wa mabasi kituoni hapo, walisema kuanzia juzi wasafiri wamepungua na hata biashara imeanza kuwa ngumu jambo lililowalazimu wengi wao kuegesha magari kituoni.
“Hakuna wasafiri ndiyo maana unaona ofisi nyingi ziko wazi, hali ilikuwa mbaya wasafiri walikuwa wengi, tulikuwa hatuhangaiki hata kupiga debe,” alisema Nuru Mtoto wakala wa mabasi ya kwenda Kaskazini.
Wakala mwingine, Kavana Mchumbichuzi alisema kwa sasa wasafiri wanakata nauli halali tofauti na ya kilanguzi kutokana na uchache wao.
Mchumbichuzi alisema mwanzoni nauli zilipanda siyo kwa matakwa yao bali wasafiri wenyewe ndiyo walitengeneza mazingira ya kupandishiwa nauli kwa sababu wengi walikuwa wanalazimisha wapate usafiri.
“Kuna watu wamesafiri kwa kulanguliwa tiketi, hasa wa kaskazini kutoa Sh100,000 kwa wakala amkatie tiketi haoni shida ili mradi tu afike anakokwenda,” alisema wakala Mohamed Rashidi.
Meneja Usalama wa Barabarani na Mazingira kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Geoffrey Silanda alisema wasafiri wapo wachache ubungo.
Credits: Mwananchi
Mshirirkishe na mwenzako kuhusu habari hii!!
Ubungo hali ni shwari sasa, swala la ULANGUZI WA TIKETI limekwisha!!!
Reviewed by Zero Degree
on
12/27/2015 02:59:00 PM
Rating: