Watu 20 wauawa kwa bomu lililolipuka msikitini.
Magari yakiungua wakati wa mlipuko huo.
WATU wapatao 20 wanasemekana kufa huko Maiduguri, Jimbo la Borno nchini Nigeria baada ya bomu kulipuka msikitini leo.
Kwa mujibu wa gazeti la Premium Times, wengi wa waliouawa wanaaminika ni wakazi wa eneo hilo ambao walikuwa wamekusanyika katika msikitu huo kufuatia uvumi kwamba kulikuwa na bomu lililokuwa limeachwa humo.

“Sijaona kitu cha kipumbavu kama hiki ambapo watu waliingia katika msikiti kuchunguza iwapo kweli kulikuwa na bomu. Kweli bomu lilikuwemo na likalipuka na kuua watu zaidi ya 20 na wengi kujeruhiwa,” alisema ofisa mmoja wa polisi akiongea na gazeti hilo.
Hata hivyo, mmoja wa wakazi wa eneo hilo, alisema ni kawaida kwa wakazi wake kukusanyika eneo la msikiti kila asubuhi.
“Watu hukaa eneo la msikiti kila asubuhi ambapo kwa ajili ya maongezi na kupumzika,” alisema mkazi mmoja na kuongeza kwamba bomu hilo lilikuwa si la kujitoa mhanga bali liliwekwa makusudi na watu fulani.
Shambulizi la wapiganaji wa Boko Haram jana liliua watu 15 wa familia moja baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa na mabomu kujilipua baada ya familia hiyo kumkaribisha nyumbani kwao wakiamini alikuwa anakimbia magaidi.

Credits: GPL
Comment & Share this story!!
Comment & Share this story!!
Watu 20 wauawa kwa bomu lililolipuka msikitini.
Reviewed by Zero Degree
on
12/28/2015 06:39:00 PM
Rating: