UKATILI kwa Watoto wazidi kushika kasi.
Vilevile utafiti umebaini kuwa asilimia 75 ya watoto wenye umri huo, wamefanyiwa ukatilu wa kimwili na asilimia 25 wa kisaikolojia.
Hayo yalibainika mwishoni mwa wiki wakati Shirika lisilokuwa la Kiserikali la C-sema lilipotoa matokeo ya huduma ya simu kwa watoto wenye umri huo wanaofanyiwa vitendo vya unyayasaji katika jamii.
Msimamizi wa Kituo cha huduma ya simu kwa watoto kutoka Shirika la C-Sema, Thelma Dhaje alisema kuanzia 2013 hadi Desemba mwaka huu, wamepokea simu 7,000, 3,017 kati ya hizo zilikuwa zinahusu ukatili wa watoto ikiwamo kubakwa, kupigwa na kuachishwa masomo.
Alisema asilimia 85 ya watoto wenye umri kati ya miaka 13 hadi 24 wamefanyiwa ukatili wa aina zote na asilimia 40 wa kingono, asilimia 25 wa kisaikolojia.
Ofisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Temeke, Subsiya Kabuje alisema manispaa hiyo imeokoa watoto 178 waliokuwa kwenye mazingira hatarishi kupitia mfumo wa mabadiliko ya tabia kwa watoto.
Awali, Mwakilishi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mariam Nkumbwa, alisema Halmashauri 181 nchini zimepelekewa fedha na kwamba, halmashauri hizo ndizo zilizoanzisha Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe.
Credits: Mwananchi
Comment & Share this story!!
UKATILI kwa Watoto wazidi kushika kasi.
Reviewed by Zero Degree
on
12/28/2015 06:52:00 PM
Rating: