Loading...

Waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye akanusha kukataza kuvaa mavazi ya kubana.


Waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye.
Waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye, amekanusha taarifa iliyosambaa mitandaoni inayohusu wizara yake kukataza baadhi ya mavazi hasa sehemu za mikusanyiko ya umma.

Amesema Taarifa hizo ni za uzushi na uongo, na kuwataka mamlaka husika kuwachukulia hatua watu waliotoa taarifa za uongo.

“Hizo taarifa ni uzushi mtupu na uongo, mamlaka husika wachukue hatua, watimize wajibu wao, watumie sheria iliyopo kuwachukulia hatua”, amesema Mh. Nape Nnauye.

Mwishoni mwa wiki hii kuna taarifa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha ni taarifa kwa vyombo habari juu ya katazo la mavazi yasiyofaa kwenye mikusanyiko ya watu, hususan hospitali, maofisini, sokoni, na vyuoni.



Credits: Global publishers


Comment & Share this story!!

Waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye akanusha kukataza kuvaa mavazi ya kubana. Waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye akanusha kukataza kuvaa mavazi ya kubana. Reviewed by Zero Degree on 12/28/2015 04:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.