Loading...

Diego Costa akimbizwa hospitali.


London, England. Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa amekimbizwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi katika ugoko wake kutokana na maumivu aliyoyapata katika mchezo wa Jumamosi wa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Everton.

Nyota huyo wa miaka 27 alifunga bao moja kati ya matatu na kutoa pasi ya bao la pili, lakini alitoka dakika ya 80 baada ya kutibiwa kwa muda mrefu uwanjani bila mafanikio.

Costa amefunga mabao matano katika mechi tano tangu kuja kwa kocha mpya, Guus Hiddink katika kikosi cha Blues, ambaye anakiongoza kwa muda tangu Desemba.

“Bado hatujajua nini kinamsumbua katika ugoko wake, lakini naamini si tatizo kubwa,” alisema Hiddink.

“Alikuwa katika maumivu makali baada ya kugongana na mchezaji wa Everton,” alisema Hiddink.

Costa alikuwa mfungaji bora wa Chelsea msimu uliopita baada ya kufunga mabao 20, wakati Chelsea ikitwaa taji la Ligi Kuu na Kombe la Ligi.


Source: Mwananchi
Diego Costa akimbizwa hospitali. Diego Costa akimbizwa hospitali. Reviewed by Zero Degree on 1/18/2016 06:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.