Loading...

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru Philip Saliboko.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Philip Saliboko.



Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru Ofisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Philip Saliboko baada ya kumuona hana hatia katika tuhuma za kupokea rushwa ya Sh40.4 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa zamani wa IPTL, James Rugemalira.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema Mahakama imemuachia huru Saliboko baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi yake pasipo kuacha shaka yoyote.

Hakimu alisema licha ya kumwachia huru, upande ambao haujaridhika unaweza kukata rufani.

Alisema mshtakiwa huyo aliposomewa shtaka kwa mara ya kwanza alikana na kwamba, wakati wa usikilizwaji Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dennis Lekayo alipeleka mashahidi watatu.

Saliboko aliyekuwa anatetewa wa Wakili Jamhuri Johnson wakati wa kujitetea alifanya hivyo mwenyewe.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu alisema shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka ambaye alikuwa mpelelezi mkuu, Emmanuel Koroso, alieleza kwamba alijiridhisha kuwa fedha hizo ziliingizwa katika akaunti ya Saliboko na pia hakuwa na maelezo mazuri kuonyesha namna alivyozipokea.

Hakimu huyo alisema mashahidi wawili kutoka Benki ya Mkombozi walithibitisha Saliboko alifungua akaunti kama mteja wao na fedha hizo ziliingizwa katika akaunti yake na kuzitoa mara tatu,

Saliboko alikubali kufungua akaunti katika benki hiyo na kuingiziwa fedha hizo na Rugemalira ambaye alikuwa na makubaliano naye ya kumtafutia shamba katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam ili aendeleze biashara zake. 


Hakimu alisema kwa mujibu wa Sheria za Takukuru mtoa rushwa na mpokeaji wote ni wakosaji na kuhoji kama kweli ilikuwa rushwa kwa nini Rugemarila hakupelekwa mahakamani kushtakiwa maana ni mtoaji.




ZeroDegree.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru Philip Saliboko. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru Philip Saliboko. Reviewed by Zero Degree on 1/30/2016 02:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.