Msajili wa Vyama vya siasa awajibu BAVICHA Wanaotaka CCM Ifutiwe Usajili Kwa Ubaguzi.
Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi alisema kuwa hawezi kuwazuia Bavicha kumpeleka mahakamani kwani hiyo ni haki yao. Lakini akawashauri kuwa kabla hawajazungumza walichozungumza ni vyema kwanza wangemuuliza na kuwa na uhakika kwani tayari ameshachukua hatua za kisheria dhidi ya CCM.
“Wanatakiwa kuwa na uhakika kwanza,” alisema Jaji Mutungi. “Mimi nimeshawachukulia hatua CCM, tena hatua kwa mujibu wa sheria. Nimewaandikia barua nikiwataka wajieleze kuhusu ujumbe huo wa kibaguzi ulioonekana,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Jaji Mutungi alisema kuwa tayari ofisi yake imeshaingilia mgogoro wa uchaguzi unaoendelea visiwani Zanzibar kwa kuwa unawahusu wadau ambao ni vyama vya siasa.
Alisema amezungumza na pande mbili zinazozozana ili kusaidia katika kupata maridhiano ya amani.
ZeroDegree.
Msajili wa Vyama vya siasa awajibu BAVICHA Wanaotaka CCM Ifutiwe Usajili Kwa Ubaguzi.
Reviewed by Zero Degree
on
1/19/2016 12:13:00 PM
Rating: