NEMC yakwaa kisiki kwa Rwakatare.
Uamuzi huo ulitolewa juzi na Jaji, John Mugeta baada ya wakili wake, Emmanuel Muga kuwasilisha maombi mahakamani hapo chini ya hati ya dharura, akiomba zuio la kuvunjwa kwa nyumba hiyo mali ya mtoto wa mchungaji huyo, Robert Brighton.
Brighton kupitia wakili wake waliwasilisha maombi hayo baada ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuiwekea alama ya X na kumtaka mmiliki aibomoe kwa hiyari kabla hatua zaidi hazijachukuliwa.
Jaji Mugeta alisema pande husika zilikuwa na kesi namba 70 ya mwaka 2012 iliyotolewa hukumu na kumpa haki Brighton huku akisisitiza hakuna kuchukuliwa hatua nyingine yoyote dhidi ya jengo hilo.
Katika kesi hiyo, nyumba hiyo inadaiwa kuwa ipo kwenye ramani ya mipango miji iliyopimwa kama viwanja namba 2019 na 2020 ambavyo hati yake ilitolewa kwa mara ya kwanza 1979.
Ilidaiwa kuwa mwaka 2011, NEMC ilitoa taarifa ya kuvunja nyumba hiyo kwa kushinikizwa na wakazi wa eneo hilo baada ya kuona ujenzi unaanza wakidhani utaziba mto Ndumbwa ambao hauendelei.
Pia, nyumba hiyo ilidaiwa kuwa ipo karibu na mikoko, kitu ambacho kinapingwa na Brighton kupitia wakili wake Muga.
Source: Mwananchi
Comment & Share this!!
NEMC yakwaa kisiki kwa Rwakatare.
Reviewed by Zero Degree
on
1/07/2016 01:30:00 PM
Rating: