Loading...

Paul Chagonja Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.


Paul Chagonja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wawili wa mikoa ya Mwanza na Katavi ili kujaza nafasi za Makatibu Tawala wa mikoa hiyo.


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais amemteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Mtweve alikuwa Kamishna wa fedha na Utawala wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Balozi Sefue amesema Rais Magufuli pia amemteua Kamishna wa polisiPaul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Chagonja alikuwa Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Aidha, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli ameamua kuwateua Makamishna hawa wa Polisi kama alivyowateua Majenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.

Makamishna Clodwing Mtweve na Paul Chagonja pamoja na Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Kuwait, wataapishwa kesho Jumamosi tarehe 30 Januari, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, saa nne asubuhi.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam.
29 Januari, 2016




ZeroDegree.
Paul Chagonja Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi. Paul Chagonja Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi. Reviewed by Zero Degree on 1/29/2016 07:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.