Loading...

Sengerema: Mgogoro mkubwa wazuka baina ya wananchi na mtu [ mwenyekiti wa serikali ya kijiji ] aliyejimilikisha mlima kama eneo lake, pata undani wa mgogoro huo hapa.


Mwanza. Wakazi wa Kitongoji cha Kigoto, wameuomba uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kuingilia kati mgogoro kati yao na mwenyekiti wa serikali ya kijiji baada ya kuzuiwa kulisha mifugo yao kwenye eneo la mbuga na kuligeuza mali yake.



Pia, walimuomba Mkuu wa wilaya hiyo, Zainab Telack kuingilia kati kwa kufuatilia mmiliki wa eneo lilipo karibu na Mlima Lwepisi, ambao mwenyekiti huyo anadaiwa kutumia kwa shughuli za uzalishaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema eneo hilo walikuwa walikitumia kulisha mifugo yao, lakini baada ya mwenyekiti kuapishwa alianza kuwawekea vikwazo.

Mwenyekiti huyo, Tiba Magambo alikanusha kuzuia mbuga hiyo kwa lengo la kuifanya eneo la hifadhi la kijiji na kuliepusha kuvamiwa na wajanja.

Kuhusu suala la eneo la mlima, Magambo alisema kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi, siyo miliki ya mtu, hivyo alizuia ili uendelee kuwa hifadhi ya kijiji.

Naye Tiba Nsiyonka anayedai mmiliki halali wa mlima huo, alisema mgogoro uliibuka baada ya mwenyekiti kumwandikia muhtasari wa umiliki na kuanza ujenzi wa vibanda vya ufugaji nyuki.

Mwenyekiti wa Kitogoji cha Kigoto, Mbikisa Galingulwa alisema aliandika muhtasari wa kummilikisha mlima baada ya baraza la wazee kuridhia kuwa mlima huo ulikuwa kwenye miliki yake halali.

“Niliandika muhtasari wa kumpatia mlima huo, kutokana na wazee kujiridhisha kuwa ni eneo lake,” alisema Galingulwa. Mkuu wa Wilaya Telack aliwataka wakazi hao kufika ofisini kwake Februari mosi, ili awasikilize madai yao, yakishindikana kutatuliwa watapatiwa msaada wa kisheria badala ya kuendeleza malumbano kwenye vyombo vya habari.




ZeroDegree.
Sengerema: Mgogoro mkubwa wazuka baina ya wananchi na mtu [ mwenyekiti wa serikali ya kijiji ] aliyejimilikisha mlima kama eneo lake, pata undani wa mgogoro huo hapa. Sengerema: Mgogoro mkubwa wazuka baina ya wananchi na mtu [ mwenyekiti wa serikali ya kijiji ] aliyejimilikisha mlima kama eneo lake, pata undani wa mgogoro huo hapa. Reviewed by Zero Degree on 1/30/2016 03:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.