Loading...

Shule yenye wanafunzi 416 ina walimu wawili.


Mvomero. Shule ya Msingi Tandari katika Kata ya Bunduki mkoani Morogoro ina walimu wawili wanaolazimika kufundisha wanafunzi 416 kwa zamu.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Selemani Shemsanga alisema jana kuwa tatizo la upungufu wa walimu linaikabili shule hiyo kuanzia mwaka 1943 ilipoanzishwa.

Alisema upungufu huo unawalazimu walimu hao akiwamo mkuu wa shule kufundisha kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la saba kwa zamu ili wamudu kutoa elimu kwa wanafunzi licha ya kuwapo kwa upungufu huo.

Mwalimu Shemsanga alisema upungufu huo wa walimu unawalazimu kufundisha kipindi kimoja chini ya muda wa kawaida ili waweze kuwafundisha wanafunzi wote.

Aliyataja baadhi ya masomo ambayo wamelazimika kuacha kuyafundisha kutokana na kukosekana kwa walimu kuwa ni Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Haiba na Michezo pamoja na Uraia kwa darasa la sita na saba.

Mwalimu Shemsanga alisema kama Serikali imejizatiti kuinua elimu nchini, ihakikishe inapeleka walimu na vifaa vya kufundishia kwa shule zilizopo vijijini.

Alisema pia inapaswa ifute uhamisho usio na lazima na iwape marupurupu walimu wa maeneo ya vijijini.

Mwalimu wa Taaluma, Michael Panga alisema shule hiyo kwasasa inahitaji angalau walimu tisa wa daraja A wa masomo ya sayansi na lugha kwa madarasa yote.



ZeroDegree.
Shule yenye wanafunzi 416 ina walimu wawili. Shule yenye wanafunzi 416 ina walimu wawili. Reviewed by Zero Degree on 1/19/2016 08:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.