Loading...

Suala la Rushwa nchini litabakia kuwa ndoto, serikali ya awamu ya tano yaapa.


SERIKALI ya Awamu ya Tano imesema imejipanga katika kuhakikisha inapambana na tatizo la rushwa kuanzia kwenye chanzo chake ili kuiwezesha nchi kuondokana na tatizo hilo na kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara na uwekezaji.



Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan baada ya kuzindua Mtandao wa Umoja wa Mataifa wa Global Compact, wenye lengo la kukutanisha sekta binafsi, kampuni kubwa na wafanyabiashara kwa lengo la kuboresha na kuimarisha biashara nchini.

Kupitia mtandao huo, sasa sekta binafsi inatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi 10 ya mtandao huo ambayo ni kufanya biashara kwa kuzingatia haki za binadamu, kupambana na rushwa, kukuza ajira, kutunza mazingira na kuepuka kutumikisha watoto.

Misingi mingine ni kuepuka utumikishwaji wa ajira wa aina yoyote, kuzingatia uhuru wa mfanyabiashara na kampuni husika, kuepuka unyanyasaji, biashara kuzingatia utunzaji wa mazingira, kuhamasisha juu ya utunzaji wa mazingira na biashara kuepuka mazingira ya rushwa na hongo.

Makamu wa Rais alisema kupitia mtandao huo, jamii ya wafanyabiashara inatakiwa kushiriki bega kwa bega katika mapambano dhidi ya rushwa ikiwamo kushiriki katika kutengeneza sheria na sera nzuri zitakazorahisisha vita dhidi ya tatizo hilo.

Alisema Serikali kupitia Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Shirikisho la Wafanyabiashara Tanzania inatambua kuwa ina wajibu wa kulinda haki za wananchi, ikiwemo za wafanyakazi na waajiri.

Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Global Compact Tanzania, Patrick Ngowi alisema mtandao huo ulianzishwa miaka 15 iliyopita na Umoja wa Mataifa na hadi sasa una wanachama takribani 12,000 katika nchi 162 na Tanzania kwa sasa takribani kampuni 42 zimejiunga na ina wanachama 9,000.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli hasa katika kupambana na matatizo ya rushwa.



ZeroDegree.
Suala la Rushwa nchini litabakia kuwa ndoto, serikali ya awamu ya tano yaapa. Suala la Rushwa nchini litabakia kuwa ndoto, serikali ya awamu ya tano yaapa. Reviewed by Zero Degree on 1/21/2016 01:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.