Loading...

"Subirini tarehe ya uchaguzi...", Shein awaambia Wazanzibari.


Rais Ali Mohamed Shein

Rais Ali Mohamed Shein amesema uchaguzi mkuu visiwani Zanzibar utarudiwa hivyo wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu kusubiri tarehe ya upigaji kura itakayopangwa na Tume uya Uchaguzi (ZEC).



Akihutubia katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani, Dk Shein amejivunia mafanikio ya serikali yake ambayo msingi mkuu ni mapinduzi hayo yaliyotokea visiwani humo zaidi ya miongo mitano iliyopita.

Katika maadhimisho hayo yaliyoambatana na gwaride kutoka vikosi mbalimbali vya majeshi na kuhudhuriwa na Rais John Magufuli pamoja, marais wastaafu kutoka bara na visiwani pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali, Shein amesisitiza kuwa kikatiba, ZEC ndiyo yenye dhamana ya kutangaza siku ya uchaguzi.

Hata hivyo Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif ametimiza azma yake ya kutohudhuria sherehe hizo akipinga uamuzi wa ZEC kufuta matokeo na kutaka uchaguzi urudiwe.

Akimalizia kutoa hotuba yake, Shein hakuacha kumtaja Maalim Seif kama miongoni mwa viongozi waliomsaidia katika kipindi chake cha uongozi katika visiwa hivyo maarufu duniani katika sekta ya utalii.



Source:Mwananchi
"Subirini tarehe ya uchaguzi...", Shein awaambia Wazanzibari. "Subirini tarehe ya uchaguzi...", Shein awaambia Wazanzibari. Reviewed by Zero Degree on 1/12/2016 05:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.