Loading...

Taasisi za Kitanzania zang’ara Afrika.


Mkurugenzi wa Utafiti wa Utawala bora na huduma za kijamii toka Repoa Dr Lucas Katera.

Dar es Salaam. Taasisi nne za Tanzania zinazojihusisha na tafiti mbalimbali za kiuchumi, kisera na kijamii ni miongoni mwa 92 bora Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazofanya kazi kwa viwango vya ubora, uwazi na ushawishi katika matokeo ya kazi zake.

Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylavania nchini Marekani wamekuwa wakifanya utafiti wa kuangalia ubora wa taasisi hizo na kwa mwaka huu zaidi ya 60,000 duniani zilishiriki.

Utafiti wa watalaamu hao umetoa matokeo yanayoonyesha Taasisi ya Utafiti wa Sera za Umma na Uchambuzi ya Kenya (KPPIRA) ikishika nafasi ya kwanza kwenye nchi 20 bora za Kusini mwa Afrika. Utafiti huo ulianza mwaka 2006 na ulikamilika mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa hapa nchini, Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umaskini nchini (Repoa) imeshika nafasi ya 18, Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) nafasi ya 42, Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Teknolojia (ATPS) nafasi ya 51 na ya Uongozi imeshika nafasi ya 60.

Akizungumzia matokeo ya utafiti huo ulioanza kufanyika miaka tisa iliyopita, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Repoa, Dk Donald Mmari alisema wamefarijika kupata mafanikio hayo, lakini wanakabiliwa na changamoto ya ufadhili wa bajeti kutoka serikalini kwa ajili ya kuongeza ufanisi na kasi ya ubora wa kazi zao.

“Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliahidi kabla ya kuondoka angekuwa anatenga asilimia moja kwa ajili ya kusaidia shughuli za kitafiti, lakini ahadi hiyo bado haijatekelezwa,” alisema. 

Dk Mmari alisema wanaweza kuwa bora zaidi ya mafanikio hayo endapo watapata ufadhili mzuri kwa kuwa nchi tano zilizong’ara katika utafiti huo zinafadhiliwa na Serikali zao.



ZeroDegree.
Taasisi za Kitanzania zang’ara Afrika. Taasisi za Kitanzania zang’ara Afrika. Reviewed by Zero Degree on 1/30/2016 05:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.