TANZIA: Mtunzi wa Tamthiliya ya NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE Afariki Dunia.
Dk. Edwin Semzaba enzi za uhai wake.
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwandishi wa tamthiliya ya “Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe,” Dk. Edwin Semzaba amefariki dunia jana January 17, majira ya jioni.
Taarifa kutoka ndani ya familia ya marehemu inasema kuwa, Dk. Semzaba amefariki dunia akiwa amelazwa hospitalini lakini familia hiyo hawajaweka wazi nini chanzo cha kifo cha mtunzi huyo mahiri wa vitabu tanzania.
Dk. Semzaba pia alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA ).
Jamii ya Watanzania itamkumbuka sana Dk. Edwin Semzaba kwa umahiri wake wa utunzi wa vitabu hasa kitabu cha “Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe” ambacho kilisomwa sana na mpaka sasa kinatumika sana katika kufundishia wanafunzi wa shule za sekondari hapa nchini.
Source: GPL
TANZIA: Mtunzi wa Tamthiliya ya NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE Afariki Dunia.
Reviewed by Zero Degree
on
1/18/2016 10:34:00 AM
Rating: