Loading...

TRA yaongeza muda wa mwezi mmoja wa usajili wa pikipiki.


Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imeongeza muda wa usajili wa Pikipiki hadi februari Mosi mwaka 2016.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika kikao chake cha kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi. Kaimu Kamishna Mkuu amesema wameamua kuongeza muda wa zoezi hilo ili kuwapa nafasi wale ambao bado hawajasajili.

“ Natoa wito kwa wamiliki wa pikipiki kusajili vyombo vyao mapema ili wasipatwe na adha itakayojitokeza baada ya muda uliotolewa kumalizika ” Alisema Kaimu Kamishna Kidata.

Ameongeza kuwa zoezi hilo lilikumbwa na changamoto kadhaa zilizowalazimu kuongeza muda mara mbili, ambazo ni umbali wa vituo vya usajili na makazi ya wamiliki wa pikipiki hasa mikoani,pamoja na upotevu wa nyaraka za kununulia pikipiki.

Aidha Kaimu Kamishna Alphayo Kidata ameomba wananchi kushirikiana na Mamlaka ili kutimiza azimio la Serikali ya Awamu ya Tano ya kulijenga taifa kwa kufanya kazi na hasa kulipa kodi stahiki zinazoleta mapato yanayowezesha maendeleo katika taifa letu.

Zoezi la usajili wa pikipiki lilianzishwa kwa lengo la kurahisisha ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyombo hivyo na lilipangwa kukamilika tangu Desemba 31, 2015 lakini ikaonekana wengi hawakusajili pikipiki zao hivyo basi Mamlaka imetoa mwezi mmoja mpaka Februari Mosi 2016
TRA yaongeza muda wa mwezi mmoja wa usajili wa pikipiki. TRA yaongeza muda wa mwezi mmoja wa usajili wa pikipiki. Reviewed by Zero Degree on 1/06/2016 08:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.