Loading...

Majengo ya kifahari Moshi kubomolewa.


Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga.

Moshi. Majengo ya kifahari yaliyojengwa ndani ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro yanatarajiwa kubomolewa wakati wowote kuanzia kesho.

Serikali pia bado inaendelea na kazi ya kubaini majengo mengine ya kubomolewa.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vya ndani ya Serikali, vimelidokeza gazeti hili kuwa wilaya za Hai na Moshi, ndizo zitakazo athirika zaidi.

Sheria ya Mipango miji ya Mwaka 1979, inazuia mtu yeyote kufanya shughuli za kibinadamu ikiwamo kujenga nyumba za kuishi, ndani ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji ikiwamo mito.

Hata hivyo, habari zinadai kuwa nyumba nyingi za kifahari katika wilaya hizo hususan maeneo ya Kibosho, Marangu, Old Moshi na Mwika, zimejengwa karibu na mito na zile za Moshi Mjini, nyingi zimejengwa kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.

Baadhi ya nyumba hizo zinamilikiwa na wafanyabiashara na viongozi wengine waliowahi kushika nyadhifa za juu katika taasisi nyeti serikalini.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga alipoulizwa leo, alisema bomoabomoa hiyo itaanza wakati wowote na kinachosubiriwa sasa ni utaratibu wa kuanza kazi hiyo.

“Ni kweli tunatarajia kuanza kuwabomolea wale wote waliojenga ndani ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji. “Wapo watu wamejenga makazi ya kudumu, lazima nyumba zao zivunjwe,” alisisitiza mkuu huyo wa wilaya.


Source:Mwananchi

Comment & Share this!!
Majengo ya kifahari Moshi kubomolewa. Majengo ya kifahari Moshi kubomolewa. Reviewed by Zero Degree on 1/06/2016 08:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.