Loading...

Watozwa faini ya Sh 50,000/= kwa KUTOFANYA USAFI 9 Desemba.


Rais John Pombe Magufuli akifanya usafi kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Mufindi. Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Igowole wilayani Mufindi mkoani Iringa, wameulalamikia uongozi wa kata hiyo kwa kuwakamata na kuwatoza faini ya Sh50,000 kila mmoja kwa madai ya kutofanya usafi Desemba 9 mwaka jana.

Raia John Magufuli aliahirisha sherehe za Uhuru wa Tanganyika ambazo hufanyika Desemba 9 kila mwaka nchini na kuamuru siku hiyo itumiwe kwa kufanya usafi wa mazingira.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi hao walisema licha ya kushiriki kazi ya kufanya usafi siku hiyo, bado majina yao yaliorodheshwa na kufikishwa kwenye Baraza la Migogolo la Kata walikoamriwa kulipa faini hiyo ya Sh50,000.

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Igowelo, Mario Ngubi alisema alipata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kitongoji Desemba 20, mwaka jana, akitakiwa kufika kwenye baraza la migogoro la kata kwa ajili ya kusikiliza shauri dhidi yake na wenzake.

Alisema mara alipofika kwenye ofisi ya kata, alisomewa mashtaka kuwa yeye hakufanya usafi siku ya Desemba 9 mwaka jana na hakutakiwa kujitetea badala yake alitakiwa kulipa faini.

Madai ya Ngubi yaliungwa mkono na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Muhamati, Mchungaji Erasmus Msimiyu aliyedai kuwa katika kitongoji chake wakazi 18 waliorodheshwa nao walidaiwa kuwa hawakufanya usafi, wakati walifanya kazi hiyo.

“Kuna baadhi walienda na wengine hawakwenda, lakini kuna mmoja alimpigia simu mbunge wetu Mendrad Kigola na kumweleza, aliamuru waachiwe,” alisema.

Mbunge huyo wa Mufindi Kusini, Kigola alikiri kupigiwa simu na wakazi hao kuhusiana na kero hiyo. Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Igowole, Hildfonce Kafuka alipoulizwa alijibu kwa kifupi kuwa hajui chochote.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Patrick Lalika alisema ofisi yake haina taarifa juu ya watu kulipishwa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kutoshiriki usafi.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jowika Kasunga alisema wahusuka wanaolalamikia suala hilo wanaweza kufika ofisini kwake ili hatua zaidi zichukuliwe.


Source: Mwananchi

Comment & Share this
Watozwa faini ya Sh 50,000/= kwa KUTOFANYA USAFI 9 Desemba. Watozwa faini ya Sh 50,000/= kwa KUTOFANYA USAFI 9 Desemba. Reviewed by Zero Degree on 1/11/2016 06:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.