Loading...

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, aapa kuhakikisha nidhamu kwa watumishi wa umma inarudi.


Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa,amesema serikali imeweka msisitizo katika kuhakikisha inarudisha nidhamu kwa watumishi wa umma kwa kuweka mkazo katika uadilifu, uwajibikaji, kutoa huduma kwa wakati.

Waziri mkuu Majaliwa ameyasema hayo katika mkutano wa pili kikao cha tatu Bungeni Mjini Dodoma alipokua akihitimisha hoja ya kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa siku ya ufunguzi wa Bunge la kumi na moja tarehe 20 Novemba 2015

Amesema kuwa serikali itakuwa inawakumbusha watanzania na watendaji wa serikali kufanya majukumu yao kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za haraka dhidi ya watumishi wanaokwenda kinyume na misingi ya utendaji kazi serikali kwa kuzingatia kauli mbiu ya hapa kazi tuu.

Pia amesema kuwa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge ambazo utekelezaji wake utahitaji kutengewa fedha za uandalizi wa kutenga fedha za serikali na utendaji wake utafanyika kwa haraka kwa kuzingatia maombi na hoja za wabunge kwakusimamia mapato ya Taifa ili yaongezeke kwa kiwango kikubwa.



ZeroDegree.
Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, aapa kuhakikisha nidhamu kwa watumishi wa umma inarudi. Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, aapa kuhakikisha nidhamu kwa watumishi wa umma inarudi. Reviewed by Zero Degree on 1/29/2016 05:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.